Makala
KUWA NA MOYO WA SHUKRANI
| Makala
𝐌𝐎𝐘𝐎 𝐖𝐀 𝐒𝐇𝐔𝐊𝐔𝐑𝐀𝐍𝐈
1 Nyakati 16:7
7 Ndipo siku hiyo Daudi alipoagiza kwanza kumshukuru Bwana, kwa mkono wa Asafu na nduguze.
Mfalme Daudi anawaagiza watu wake kutanguliza shukurani zao mbele za Mungu.
Kushukuru bado kunabaki kuwa ni wajibu wa msingi kwa Mkristo yoyote anayemtegemea Mungu kama Bwana na mwokozi wa maisha yake.
Kushukuru ni jambo muhimu kwasababu Mungu anapendezwa na watu wenye mioyo ya shukrani.
Mtu anayekumbuka kushukuru anaheshimiwa sana na Mungu kuliko hata anayekumbuka kuomba kila siku.
Wakolosai 3:15
15 Na amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu; ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja; tena iweni watu wa shukrani.
Kushukuru ndiko kunatuongezea mvuto kwa Bwana kuliko tunavyoendelea kukazana kuomba kila siku.
Tunaomba sana ili tupate Neema na Rehema. Kuomba ni haki yetu sawa Ila kumshukuru Mungu siku zote ndio huuchangamsha moyo wa Mungu.
Kushukuru ndiko kunakokupaa ujasiri wa kwenda kushuhudia matendo ya Bwana kwa mataifa.
Kushukuru ndiko kunakompa Mungu nguvu ya kuendelea kushughulika na mambo yako, mtu anayemshukuru Mungu kwa matendo yake makuu. Miujiza na maajabu havitaondoka nyumbani kwake.
Yeremia 30:19
19 Tena kwao itasikiwa shukrani, na sauti yao wachangamkao; nami nitawazidisha, wala hawatakuwa wachache; tena nitawatukuza, wala hawatakuwa wanyonge.
Kushukuru ni kama Mtaji unaokupandisha juu kwenye level za kujibiwa maombi yako,,
Kiuhalisia kushukuru kunapaswa kutangulia ndipo na maombi mengine yafuate nyuma.. Hebu Angalia una afya, unapumua, una amani, una kazi, una ndoa, una familia, kwanini usiwe unashukuru kwanza kabla ya kupeleka haja zako mbele za Mungu!
Kushukuru kunapaswa kuwa kama vazi la thamani ndani ya moyo wako kwamba usipolivaa hujisikii kama moyoni umekamilika.
Moyo wa shukrani ni kama kinanda chenye sauti nzuri masikioni mwa Mungu.,,,, Shukuru kwa kila jambo na kwa kumaanisha bila kujali yanaumiza au kufurahisha moyo wako.
1 wathesalonike 5:18
18 Shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo.
SADAKA